Lazio imemfuta kazi aliyekuwa kocha wake mkuu Stefano Pioli baada jana jumapili kufungwa mabao 4-1 na mahasimu wao wakubwa wa jiji la Roma,AS Roma.
Taarifa za ndani zinadai tayari Lazio imemteua nyota wake wa zamani Simone Inzaghi kuwa kocha wake wa muda mpaka mwisho wa msimu.
Katika mchezo wa jana Lazio ilipoteza kwa mabao ya Stephan El Shaarawy,Edin Dzeko,Alessandro Florenzi na Diego Perotti.
Kichapo hicho cha AS Roma kimeifanya AS Lazio ishuke mpaka nafasi ya nane ya msimamo wa ligi ya Seria A inayoongozwa na Juventus.
0 comments:
Post a Comment