Manchester, England.
MANCHESTER CITY imerejea nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka England baada ya Jumanne usiku ikiwa nyumbani Etihad kuifunga West Brom mabao 3-1.
Shukrani kwa mabao ya Gabriel de Jesus, Kevin de Bruyne na mkongwe Yaya
Toure.Bao la West Brom limefungwa na staa wa Wales, Hal Robson-Kanu.
Ushindi huo umeifanya Manchester City ifikishe pointi 75 na kukaa nafasi ya tatu ikiishusha Liverpool mpaka nafasi ya nne.Mchezo ujao Manchester City itakuwa ugenini kucheza na Watford.
0 comments:
Post a Comment