728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 21, 2017

    Guinea yaifuata Ghana nusu fainali AFCON U17,Cameroon yatupwa nje licha ya kushinda,Serengeti Boys kibaruani tena


    Libreville,Gabon.

    GUINEA imekuwa timu ya pili kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya vijana ya AFCON baada ya Jumamosi usiku kuwabana wababe Ghana na kutoka nao suluhu ya bila kufungana kwenye mchezo wa mwisho wa kundi A uliochezwa kwenye uwanja wa Stade de l'Amitie,Libreville.

    Suluhu hiyo imeifanya Guinea imelize michezo yake ikiwa katika nafasi ya pili baada ya kujikusanyia alama tano nyuma ya vinara Ghana weye alama saba baada ya kushuka dimbani mara tatu.

    Katika mchezo mwingine wa kundi A,Cameroon waliwafunga wenyeji Gabon bao 1-0 huko Port Gentil kwa bao la Stephane Thierry Zobo.Ushindi huo umeifanya Cameroon imalize katika nafasi ya tatu katika kundi hilo na kutupwa nje ya michuano.

    Leo Jumapili michezo ya kundi B itakwenda kuhitimishwa ambapo vinara wa kundi hilo Mali watavaana na Angola huko Libreville. Tanzania,Serengeti Boys watakuwa Port-Gentil kucheza na Niger.

    Tanzania na Mali zote zina alama nne hivyo ushindi ama sare yoyote ile itazihakikishia nafasi ya kutinga nusu fainali pamoja na kombe la dunia la vijana litakalofanyika mwezi Octoba mwaka huu huko India.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Guinea yaifuata Ghana nusu fainali AFCON U17,Cameroon yatupwa nje licha ya kushinda,Serengeti Boys kibaruani tena Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top