Barcelona,Hispania.
MLINDA Mlango wa Ujerumani,Marc-Andre ter Stegen amekubali mkataba mpya wa miaka mitano wa kuendelea kuitumikia klabu yake ya Barcelona.
Taarifa kutoka nchini Hispania zinasema kesho Jumanne,Ter Stegen atatia saini mkataba huo utakaomweka Camp Nou mpaka Juni 30,2022.
Mkataba huo pia utakuwa na kipengele kitakachomruhusu Ter Stegen kuihama Barcelona kwa ada ya uhamisho ya Euro Milioni 180 (£156m).
Ter Stegen alijiunga na Barcelona mwaka 2014 akitokea Borussia Monchengladbach.Mpaka sasa amefanikiwa kuichezea Barcelona michezo 93 na kutwaa vikombe vinane.
0 comments:
Post a Comment