Pretoria,Afrika Kusini.
YASSINE Khensissi akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga mabao mawili na kuiwezesha Esperance du Tunis ya Tunisia kuwafunga mabingwa watetezi Mamelodi Sundowns mabao 2-1 katika mchezo wa kundi C wa michuano ya klabu bingwa Afrika uliochezwa kwenye uwanja wa Lucas Moripe,Pretoria-Afrika Kusini.
Bao la kufutia machozi la Mamelodi Sundowns limefungwa na Sibusiso Vilakazi.Ushindi huo umeifanya Esperance du Tunis ikae kileleni mwa msimamo wa kundi C baada ya kufikisha pointi 7.Pointi 3 mbele ya Mamelodi Sundowns inayoshika nafasi ya pili na pointi zake 4.
Mchezo mwingine wa kundi C utachezwa kesho Jumapili ambapo AS Vita Club ya DR Congo itasafiri kwenda Addis Ababa,Ethiopia kuvaana na St. George.
0 comments:
Post a Comment