728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 03, 2017

    Mwamuzi aliyeruhusu bao la 'Mkono wa Mungu' afariki dunia



    Sophia, Bulgaria.

    MWAMUZI msaidizi raia wa Bulgaria,Bogdan Dochev aliyeshindwa kuliona bao la 'Mkono wa Mungu' la Diego Maradona kwenye mchezo wa robo fainali wa Kombe la Dunia la mwaka 1986, kati ya Argentina na England, amefariki dunia akiwa na miaka 80.

    Katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Azteca huko Mexico ilishuhudiwa Argentina ikiibuka kidedea kwa kuifunga England mabao 2-1.Mabao yote ya Argentina yalifungwa na Maradona.

    Baada ya kufunga bao la kwanza kwa mkono,Maradona alifunga bao la pili
    kwa kuwalamba chenga mabeki watano wa England kabla ya kumfunga kirahisi kipa bora wa wakati huo, Peter Shilton.

    Baada ya bao la mkono picha za TV zilimuonyesha mwamuzi Mtunisia Ali Bin Nasser akikimbia kidogokidogo kurudi katikati ya uwanja huku akimtazama Dochev. Hata hivyo Mbulgaria huyo hakuonyesha ishara yoyote kuwa bao hilo halikuwa halali.

    "Japokuwa nilihisi kuna kitu hakikuwa sawa, lakini wakati ule Fifa ilikuwa hairuhusu mwamuzi msaidizi kujadiliana lolote na mwamuzi wa kati," Dochev aliviambia vyombo vya habari vya Bulgaria miaka mitatu iliyopita.

    Lakini, Bin Nassir alikuwa na mtazamo tofauti kwa jambo hilo: "Nilikuwa nasubili Dochev anipe ishara juu ya nini kilichotokea, lakini hakuonyesha ishara kuwa kuna mtu ameshika.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Mwamuzi aliyeruhusu bao la 'Mkono wa Mungu' afariki dunia Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top