728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 03, 2017

    Hat-trick ya Giroud yamaliza gundu la miaka 17 Ufaransa


    Rennes,Ufaransa.

    MSHAMBULIAJI Olivier Giroud (Pichani) akishangilia moja kati ya mabao yake matatu (hat-trick) aliyoifungia Ufaransa jana Ijumaa usiku kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Paraguay katika ushindi wa mabao 5-0 huko Stade de la Route-de-Lorient,Rennes.

    Giroud anayeichezea Arsenal alifunga mabao hayo katika dakika za 6, 13 na 69 na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza kuifungia Ufaransa mabao matatu ( hat-trick) katika kipindi cha miaka 17.



    Mchezaji wa mwisho kuifungia Ufaransa mabao matatu ( hat-trick) alikuwa ni David Trezeguet hiyo ikiwa ni mwaka 2000 dhidi ya kikosi cha Fifa XI.

    Mabao mengine ya Ufaransa kwenye mchezo wa jana yalifungwa na kiungo wa Tottenham,Moussa Sissoko katika dakika ya 76 na mshambuliaji wa Atletico Madrid,Antoine Griezmann katika dakika ya 76.

    Ufaransa itarejea tena dimbani Ijumaa ijayo kuvaana na Sweden kwenye mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la dunia.Juni 13 itakuwa Wembley kucheza mchezo wa kirafiki na England. 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Hat-trick ya Giroud yamaliza gundu la miaka 17 Ufaransa Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top