728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 18, 2016

    HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI JUMAMOSI YA LEO JUNI 18,2016

    Martin Skrtel

    Pogba:Juventus imesema vilabu vyote vinavyomtaka kiungo wake Mfaransa,Paul Labile Pogba,23,vijiandae kutoa kitita cha €160m vinginevyo staa huyo ataendelea kubakia Turin.(AS)

    Mendy:Kiungo wa Nice Nampalys Mendy wiki ijayo atasafiri kuelekea England kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya tayari kujiunga na Leicester City. Leicester City inamuona Mendy,23,kama mbadala sahihi wa NG'olo Kante ikiwa ataamua kuondoka King Power. (L'Equipe)

    Giaccherini:Mshambuliaji wa Sunderland, Muitaliano Emanuele Giaccherini anaweza kujiunga na Chelsea msimu ujao hii ni kwa mujibu wa wakala wake Furio Valcareggi kutokana na kuwa na mahusiano mazuri na Meneja wa klabu hiyo Antonio Conte.(SportItalia)

    Skrtel:Mlinzi wa Liverpool Martin Skrtel,30, huenda akajiunga na AS Roma baada ya ripoti kutoka Italia kudai kuwa staa huyo wa Slovakia amekubali mkataba wa miaka mitatu kutua Estadio Olympico.(Gazzetta dello Sport)

    Debuchy:Besiktas inataka kumsajili kwa mkopo wa msimu mmoja mlinzi wa kulia wa Arsenal Mfaransa Mathieu Debuchy,30, kisha kumsajili moja kwa moja ikiwa ataonyesha kiwango kizuri.Debuchy,30,ameichezea Arsenal michezo 12 tangu alipojiunga nayo 2014 akitokea Newcastle United.(Sabha)

    Cassierra:Ajax imemsajili mshambuliaji wa Colombia,Mateo Cassierra kutoka  Deportivo Cali FC kwa mkataba wa miaka mitano.(Daily Mail)

    Keane:Leicester City imetuma ofa ya £10m kwenda Burnley kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa kati ya klabu hiyo Michael Keane.Keane, 23, alijiunga na Burnley mwaka 2015 akitokea Manchester United.(Mirror)

    Morata:Alvaro Morata,23, ameiambia Real Madrid kama itaamua kumnunua kutoka Juventus basi angependelea kubakia Bernabeu kupigania namba kikosi cha kwanza badala ya kuuzwa katika vilabu vingine.(AS)

    Gonzalo: Atletico Madrid imeripotiwa kuwa tayari kutuma ofa €60m kwenda Napoli ili kujaribu kumsajili mshambuliaji Muargentina Gonzalo Higuain,28,aliyefunga mabao 36 katika ligi ya Seria A msimu uliopita.(Corriere dello Sport)

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI JUMAMOSI YA LEO JUNI 18,2016 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top