728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 18, 2016

    KLABU BINGWA AFRIKA:AL AHLY CHALI KWA ZESCO UNITED

    Ndola,Zambia.

    MIAMBA ya soka ya Misri,Al Ahly imeianza vibaya michezo ya hatua ya makundi ya michuano ya kombe la klabu bingwa baada ya jioni ya leo kuchapwa mabao 3-2 na Zesco United ya Zambia katika mchezo mkali wa Kundi A uliochezwa katika uwanja wa Levy Mwanawasa ulioko mjini Ndola,Zambia.

    Mabao ya washindi Zesco United yamefungwa na George Ching’andu aliyefunga mabao mawili na dakika za 27 na 56 na Cletus Chama aliyefunga bao moja dakika ya 49 huku mabao yote ya Al Ahly yakifungwa na Mghana John Antwi dakika za 31 na 68.

    Kichapo hicho ni cha kwanza kwa Al Ahly kukipata katika mchezo wa ufunguzi wa hatua ya makundi tangu mwaka 2006 ilipochapwa na Sfaxien ya Tunisia.

    VIKOSI

    ZESCO: Nyangu Lameck, Mayembe Shemmy,Oluwafemi Ayo, Mtonga Kondwani, Odhiambo Owino, Chama Chota Clatous, Agay Anthony Akumu, Mwanza Jackson (Lazarous Kambole 66), Mwape Mwelwa (Simon Silwimba 77),Ching'andu John ( Dauti Musekwa 90+2),Misheck Chaila

    Ahly: Sherif Ekrami, Sabri Rahil (Emad Meteb 71), Ahmed Hegazy, Rami Rabia, Ahmed Fathi,Hossam Ashour (Amr El-Sulaya 60), Saleh Gomaa (Walid Soliman 62),Hossam Ghaly,Moemen Zakareya, Ramadan Sobhi, John Antwi


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KLABU BINGWA AFRIKA:AL AHLY CHALI KWA ZESCO UNITED Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top