728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 04, 2016

    UGANDA YAKARIBIA KUFUZU AFCON

    Kampala,Uganda.

    TIMU ya taifa ya Uganda imejiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu michuano ya AFCON hapo mwakani huko Gabon baada ya leo jioni kuichapa Botswana kwa mabao 2-1 katika mchezo mkali wa Kundi D uliochezwa huko Francistown.

    Mabao yaliyoipa Uganda ushindi huo muhimu yamefungwa na Kizito Luwagga pamoja na Khalid Aucho huku lile la Botswana likifungwa na Onkabetsi Makgantai.

    Ushindi huo umeipeleka Uganda mpaka kileleni mwa kundi D baada ya kufikisha pointi 10,pointi tatu zaidi ya Burkina Faso itakayocheza na Comoro kesho Jumapili.

    Matokeo hayo yameipa Uganda mwanya wa kufuzu ikiwa itaifunga Comoro katika mchezo wa mwisho hapo mwezi Septemba huku Burkina Faso ikishindwa kupata matokeo mazuri katika michezo yake miwili iliyosalia.

    Aidha hata kama Burkina Faso itashinda michezo yote na kuongoza kundi ,Uganda itafuzu kama mshindi wa pili aliyefanya vizuri (Best Loser)


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: UGANDA YAKARIBIA KUFUZU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top