728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 04, 2016

    HIZI HAPA HABARI ZA USAJILI TOKA ENGLAND JIONI YA LEO JUMAMOSI JUNI 4,2016.

    Wilshere and Vardy

    Hector: FC Cologne imefikia makubaliano na Liverpool kwa ajili ya kumuuza mlinzi wake wa kushoto Jonas Hector,26.Taarifa zaidi zinasema tayari Liverpool imeshapewa ruhusa ya kuanza mazungumzo na mlinzi huyo anayeichezea pia timu ya taifa ya Ujerumani.Ikiwa usajili huo utafanikiwa Hector atakuwa mcheza wa tatu kutoka Ujerumani kujiunga na Liverpool katika kipindi hiki cha usajili baada ya Joel Matip na Loris Karius.(Liverpool Echo)

    Rebekah:Rebekah Vardy ambaye ni mke wa mshambuliani wa Leceister City Jamie Vardy kupitia ukurasa wake wa Twitter amekanusha tuhuma zinazodai kuwa amemshawishi mme wake huyo aamue kuhamia Arsenal.Rebekah ametoa utetezi huo baada ya mashabiki wa Leceister City kumtusi kupitia mitandao ya kijamii.Wakati huohuo taarifa zinadai Jack Wilshere ndiye aliyemshawishi Vardy.(The Guardian)

    Ibrahimovic:Meneja wa Swideni Erik Hamren amefichua kwamba nahodha wa timu hiyo Zlatan Ibrahimovic,34,anaweza kupewa ruhusa muda wowote kuanzia sasa ili akakamilishe taratibu za kujiunga na Manchester United.(Goal.Com)

    Sakho:Sunderland imetuma ofa rasmi ya £11m kwenda West Ham ili kumsajili mshambuliaji wa Msenegal Diafra Sakho,26.(The Sun)

    Toure:Kiungo wa Manchester City Muivory Coast Yaya Toure ameripotiwa kuwa hivi karibuni amekataa ofa toka vilabu vya China ili kusubiri ofa toka Inter Milan ya Italia.(Sportitalia)

    Pogba:Meneja wa Manchester City Mhispania Pep Guardiola ameripotiwa  kuwa hana mpango wa kumsajili kiungo wa Juventus Mfaransa Paul Pogba,23, katika kipindi hiki cha usajili na badala yake ataelekeza nguvu zake kumsajili mlinzi wa kulia wa Arsenal Muhispania Hector Bellerin.(Manchester Evening)

    Gomes:Manchester United imeripotiwa kutuma ofa ya £35.2m kisha £11.7 hapo baadae ili kumsajili kiungo wa Valencia Mreno Andre
    Gomes Gomes,22,ameifungia Valencia mabao tisa katika michezo 77.( Daily Mail.)

    Koeman:Meneja wa Southampton Mholanzi Ronald Koeman amekubali kuwa meneja mpya wa Everton hii ni baada ya leo Jumamosi kufanya mazungumzo na wakuu wa klabu hiyo Bill Kenwright na Farhad Moshiri.(Daily Mail)



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI ZA USAJILI TOKA ENGLAND JIONI YA LEO JUMAMOSI JUNI 4,2016. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top