728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 04, 2016

    MISRI YAICHAPA TAIFA STARS NA KUFUZU AFCON,BURUNDI NAYO CHALI

    Dar es Salaam,Tanzania.

    TIMU ya taifa ya Misri imekata tiketi ya kucheza michuano ya AFCON mwakani nchini Gabon baada ya jioni ya leo kuichapa timu ya taifa ya Tanzania "Taifa Stars" kwa mabao 2-0 katika mchezo mkali wa kundi G uliochezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

    Mabao yaliyoipa ushindi Misri yamefungwa na winga wa AS Roma,Mohammed Salah dakika za 43 na 58 huku kwa upande wa Taifa Stars nahodha wake Mbwana Samatta akikosa mkwaju wa penati.

    Kwa matokeo hayo Misri imefuzu baada kufikisha pointi 7 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine za kundi G.Nigeria ina pointi 2 wakati Tanzania iko mkiani ikiwa na pointi 1.

    Katika mchezo mwingine wa kusaka tiketi ya kufuzu AFCON,Burundi ikiwa nyumbani imechapwa na Senegal mabao 2-0 katika mchezo wa Kundi K uliochezwa jijini Bujumbura.

    Mabao ya Senegal yamefungwa na Mame Biram Diof na Sadio Mane.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MISRI YAICHAPA TAIFA STARS NA KUFUZU AFCON,BURUNDI NAYO CHALI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top