Paris,Ufaransa.
WACHEZAJI wa AS Monaco wakishangilia baada ya usiku huu kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligue 1 kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2000,miaka 17 iliyopita hii ni kufuatia ushindi wao wa mabao 2-0 nyumbani Stade Louis II dhidi ya wageni wao Saint-Etienne.
Mchezaji bora chipukizi wa mwaka,Kylian Mbappe aliiandikia AS Monaco bao la kwanza katika dakika ya 19 kabla ya Valere Germain kufunga la pili katika dakika ya 93 na kuipa miamba hiyo ubingwa wake wa nane wa Ligue 1 na kuhitimisha ufalme wa mahasimu wao Paris Saint-Germain ambao wamekuwa wababe katika miaka ya hivi karibuni.
REKODI
AS Monaco imefunga mabao 103 katika michezo 37.
Ubingwa:2017,2000,1997,1988,1982,1978,1963,1961.
0 comments:
Post a Comment