Gentil,Gabon.
GHANA imekuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya AFCON ya vijana wa U17 na timu ya kwanza kufuzu kombe la dunia la wachezaji wa umri huo baada ya Jumatano usiku kuwafunga wenyeji Gabon mabao 5-0 kwenye mchezo wa kundi A huko Stade de Port-Gentil.
Mabao yaliyoandikisha ushindi huo mnono kwa Ghana yamefungwa na nahodha Eric Ayiah aliyefunga mabao mawili,Emmanuel Toku aliyefunga mabao mawili pia pamoja na Patmos Arhin aliyefunga bao moja akitokea benchi.
Ushindi huo umeifanya Ghana ifikishe pointi sita baada ya kucheza michezo miwili na hivyo kuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya AFCON ya vijana wa U17 na timu ya kwanza kufuzu kombe la dunia la vijana litakalofanyika mwezi Octoba nchini India.
Ghana mabingwa wa kombe la dunia 1995 na1999 watahitimisha michezo yao Jumamosi Mei 20 kwa kucheza na Guinea huko Libreville kwenye uwanja Wa Stade de l'Amitié Sino.
0 comments:
Post a Comment