Khartoum,Sudan.
MSHAMBULIAJI wa zamani wa vilabu vya Simba na Yanga Mganda, Hamisi ‘Diego’ Kiiza amepeleka mabao yake nchini Sudan hii ni baada ya leo Jumatano kujiunga na klabu ya Hilal El Obeid kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Kiiza mwenye umri wa miaka 27 sasa amejiunga na Hilal El Obeid akitokea klabu ya URA ya nyumbani kwao Uganda aliyojiunga nayo mwezi Januari akitokea klabu ya Free State Stars ya nchini Afrika Kusini.
Akiwa na URA,Kiiza alifanikiwa kufunga mabao sita katika michezo 10 na kutajwa kwenye orodha ya sajili bora zaidi zilizofanyika kwenye ligi kuu ya Uganda.
Akifanya mazungumzo baada ya kusaini mkataba huo,Kiiza amesema ataitumia Hilal El Obeid kama daraja la kurejea kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uganda kinachonolewa na Mserbia,Milutin ‘Micho’ Sredovic.
Kiiza ataanza kuichezea Hilal El Obeid, Mei 24 mwaka huu pale itakapoikaribisha Zesco United ya Zambia kwenye mchezo wa kundi C wa kombe la shirikisho barani Afrika.
0 comments:
Post a Comment