Liverpool,England.
MAJOGOO wa Merseyside,Liverpool wameripotiwa kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji wa Las Palmas ya Hispania, Roque Mesa Quevedo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ladbrokes News,ni kwamba msimu ujao Mesa,27, atakuwa mchezaji mpya wa Liverpool na kuhitimisha safari yake ya miaka mitano ya kuhudumu Gran Canaria.
Jina la Mesa limekuja baada ya hivi karibuni kocha wa Liverpool,Jurgen Klopp kudaiwa kuwa yuko mawindoni akisaka kiungo mbunifu lakini atakayekuwa akipatikana kwa bei chee.
Msimu huu Mesa amejizolea ujiko mkubwa Las Palmas baada ya kuichezea miamba hiyo michezo 24 na kuifungia bao moja huku akitoa pasi za mabao za kutosha.
Dau la £15m limedaiwa kuwa litatosha kumnyakuwa Mesa ambaye pia anawindwa kwa ukaribu mkubwa na vilabu vya Tottenham na Everton.
0 comments:
Post a Comment