Rustenburg,Afrika Kusini.
KIPA wa Platinum Stars ya Afrika Kusini,Mbongeni Mzimela (Pichani) usiku wa kuamkia leo Jumapili ameibuka shujaa baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Vipers SC ya Uganda katika mchezo wa marudiano wa hatua za awali wa kombe la shirikisho barani Afrika.
Katika mchezo huo uliochezwa huko Royal Bafokeng-Rustenburg,Afrika Kusini,imeshuhudiwa Mzimela akiifungia Platinum Stars mabao hayo yote kwa mikwaju ya penati iliyopatikana katika kipindi cha kwanza na cha pili.
Bao jingine la Platinum Stars iliyolazimika kumaliza mchezo ikiwa pungufu baada ya Robert Ng'ambi kutolewa uwanjani kwa kadi mbili za njano limefungwa na Ndumiso Mabena huku lile la Vipers SC likufungwa na Milton Karisa.
Kwa ushindi huo sasa Platinum Stars inasonga hatua inayofuata kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-2.Ikimbukwe katika mchezo wa awali uliochezwa jijini Kampala,wenyeji Vipers SC walishinda bao 1-0.
0 comments:
Post a Comment