728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, August 19, 2015

    CHELSEA YAIFANYIA KITU MBAYA MAN UNITED KUHUSU USAJILI WA PEDRO,VALDES ANAHUSIKA

    Unaifahamu ishu ya Pedro kutaka kuhama FC Barcelona?Unafahamu nini kinaikwamisha Man United kukamilisha usajili huu?Hakuna kingine zaidi ya Pesa.Pesa ndiyo kila kitu.Tumesikia mengi kuhusu Man United na mengi kuhusu Pedro.Sasa sikia hii toka Chelsea.Habari mpya zinadai kuwa Chelsea imeingilia kati na kuvuruga mipango ya Man United kumnasa winga huyo wa Kispania mwenye miaka 28 baada ya kuwa tayari kutoa kitita cha paundi milioni 30 ambacho FC Barcelona inakitaka ili imuachie Pedro.Kiasi ambacho Man United hawataki kukisikia.

    Kingine kinachodaiwa kukwamisha uhamisho wa Pedro kwenda Old Trafford ni amazungumzo aliyofanya hivi karibuni na mlinda mlango Victor Valdes ambaye ni majuzi tu ameonyeshwa mlango wa kutokea Man United na kocha Louis van Gaal.Kikubwa kilichojadiliwa na nyota hao ni aina ya uongozi wa kibabe wa Van Gaal.Habari za hivi punde zinadai Man United imeachana rasmi na mpango wa kumsajili nyota huyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CHELSEA YAIFANYIA KITU MBAYA MAN UNITED KUHUSU USAJILI WA PEDRO,VALDES ANAHUSIKA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top