Singida,Tanzania.
SIKU chache baada ya kupanda ligi kuu bara, Singida United imejinasibu kuwa imejipanga kuja kuleta mabadiliko ya kweli kwenye ligi hiyo kubwa zaidi nchini Tanzania.
Katibu mkuu wa timu hiyo, Abdul Sima amesema uongozi wa Singida United umepanga kuiendesha timu hiyo kisasa zaidi kwa kuifanya kuwa kampuni ambapo mashabiki watapata fursa ya kumiliki hisa badala ya kadi za uanachama ambazo hazina tija sana.
Wakati huohuo Sima ameongeza kuwa Singida United haitaacha mchezaji yoyote yule kutoka kwenye kikosi kilichoirejesha timu hiyo ligi kuu bara labda kama mchezaji ataamua kuondoka mwenyewe.
Pia Sima amesema makocha Jumanne Charles na Fred Minziro ambao wameipandisha daraja Singida United wataendelea na vibarua vyao licha ya timu hiyo juzi Ijumaa kumwajiri Mholanzi Hans Van Pluijm kuwa kocha wake mkuu.
0 comments:
Post a Comment