Kocha mkuu wa klabu ya Crystal Palace Neil Warnock anaamini kuwa winga wake Wilfred Zaha (21) ni bora kuliko nyota wengi walioko katika kikosi cha Manchester United kinachonolewa na kocha Louis Van Gaal.
Warnok anaamini kuwa Zaha aliyeko klabuni hapo kwa mkopo akitokea Manchester United alishindwa kung'ara kutokana na kujiunga na klabu hiyo akiwa bado mdogo sana hivyo isingekuwa rahisi kwake kuaminiwa.
Warnock anasema ``Namfahamu vizuri Zaha ni mchezaji mzuri sana pengine kuliko nyota wengi walioko Manchester United kwa sasa.
Makocha huwa tuna machaguo yetu nadhani kukosa nafasi kwa Zaha kulichangiwa na mambo kama hayo"
0 comments:
Post a Comment