Klabu ya Arsenal kupitia kocha wake mkuu Arsene Wenger imefanya mazungumzo ya kushitukiza na wakala wa mlinzi wa klabu ya Real Madrid Sergio Ramos.
Wakala huyo Rene Ramos ambaye ni kaka wa damu wa Ramos alikuwa London mapema wiki hii kusikiliza ofa ya Arsenal juu ya mteja na mdogo wake Sergio Ramos ambaye inasemekana hivi karibuni alikataa ofa ya miaka miwili ya kuendelea kukipiga Santiago Bernabeu na kutaka apewe zaidi vinginevyo ataondoka zake.
Baada ya kupata habari hivyo haraka Arsenal iliamua kumtafuta Rene ili iweze kumpata mlinzi huyo mahiri aje kutibu tatizo la safu ya ulinzi inayoitatiza klabu hiyo kwa kipindi kirefu.
0 comments:
Post a Comment