Mlinzi wa kulia wa klabu ya Manchester City Pablo Zabaleta ameibuka na kumwagia sifa kemkem nyota wa klabu hiyo Frank Lampard kufuatia kuisaidia klabu hiyo kuibuka na ushindi mnono wa goli 3-0 dhidi ya klabu ya Southampton katika dimba la St.Mary's juzi jumapili.
Lampard aliingia kuchukua nafasi ya winga Jesus Navas na kufanikiwa kufunga goli la tatu baada ya kupokea pasi nzuri toka kwa mshambuliaji Sergio Kun Aguero na kufikisha jumla ya magoli 174 katika ligi ya Epl.
Zabaleta akimzungumzia Lampard amesema
``Lampard ni mchezaji wa mfano kwani licha ya kushinda mataji karibu yote akiwa na Chelsea bado ni mtu asiyeacha kupambana"
``Ni mchezaji wa kwanza kuja mazoezini na wa mwisho kuondoka,anafanya mazoezi kwa nguvu sana kama kinda wa miaka 18."
0 comments:
Post a Comment