728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, December 29, 2014

    PARDEW KOCHA MPYA CRYSTAL PALACE

    Hatimaye klabu ya Crystal Palace imefanikiwa kuinasa saini ya kocha Alein Pardew 53 toka klabu ya Newcastle United kuchukua nafasi ya kocha aliyetimuliwa wiki iliyopita Neil Warnock kufuatia matokeo mabaya katika ligi.

    Pardew anatua Palace kwa mara ya pili baada ya hapo mwanzo kutua akiwa kama mchezaji na kufanikiwa kuifungia klabu hiyo jumla ya magoli manane katika misimu minne 1987-1991.

    Kuondoka kwa Pardew Newcastle kunatokana na maelewano mabovu kati yake na uongozi wa klabu hasa mmiliki wa klabu Mike Ashley ambaye anatuhumiwa kuuza wachezaji nyota.

    Palace kupitia mmiliki wake Steve Parish imekubali kuilipa Newcastle £2m kama fidia ya kumchukua Pardew.

    Pardew anaiacha Newcastle ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa goli 3-2 iliyoupata dhidi ya klabu ngumu ya Everton jana jumapili.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: PARDEW KOCHA MPYA CRYSTAL PALACE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top