Valencia,Hispania
Klabu ya Valencia imetangaza itamfungia maisha shabiki wake aliyerusha chupa na kumjeruhi nyota wa klabu ya Barcelona Lionel Messi katika mchezo wa ligi ya La Liga uliopigwa wikendi iliyopita katika dimba la Mestalla mjini Valencia.
Shabiki huyo ambaye bado hajafahamika alirusha chupa hiyo ya plastiki na kumjeruhi Messi wakati akijumuika na wenzake karibu na kibendera cha kona kusherekea goli la dakika za mwisho la kiungo Sergio Busquets lililoipa ushindi Barcelona wa goli 1-0 dhidi ya wenyeji Valencia.
Taarifa kutoka uongozi wa juu wa Valencia zinadai kuwa klabu hiyo imeshaanza uchunguzi ili kumbaini shabiki huyo na hatimaye kumfungia maisha kuingia katika mechi zote za klabu hiyo zitakazochezwa katika dimba hilo kwakuwa kitendo hicho siyo cha kiungwana.
0 comments:
Post a Comment