Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limetoa
orodha mpya ya waamuzi
linaowatambua ,Kwenye orodha hiyo kuna
jumla ya waamuzi 18 kutoka
Tanzania,miongoni mwa waamuzi hao waamuzi
11 wapya na 7 wa zamani.
Waamuzi wapya wa kati kutoka Tanzania ni
Mfaume Ali Nassor kutoka visiwani Zanzibar
pamoja na Martin Saanya kutoka Morogoro,
pia wamo waamuzi watatu wa kike ambao ni
Florentina Zabron ,Jonesia Rukyaa pamoja na
Sofia Ismail.
Kwa upande wa waamuzi wasaidizi wanaume
ni Frank John Komba na Soud Idd Lila , kwa
upande wa wanawake ni Kudura Omary
Maurice,Hellen Joseph Mduma,Dalila Jafari
Mtwana na Grace Mawala.
Waamuzi wa zamani wa Tanzania kwenye
orodha ya FIFA ,kwa upande wa wanaume ni
Israel Mujuni Nkongo na Waziri Sheha
Waziri,kwa upande wa waamuzi wasaidizi ni
Josephat Bulali,Fernand Chacha,John
Longino Kanyenye ,Ali Kinduli na Samuel
Hudson Mpenzu .
0 comments:
Post a Comment