Mabingwa wa zamani Zambia na waandalizi wa
kombe la bara Afrika Equitorial Guinea ni
miongoni mwa timu zitakazoorodheshwa
katika droo ya kombe hilo la mwaka 2015
Jumatano usiku.
Shirikisho la soka barani Afrika CAF tayari
limezigawanya timu hizo 16 katika makundi
vyungu vinne vya kinyang'anyiro hicho cha
january 17 hadi februari 8.
Hatua hio ilifanyika kulingana na utendaji wa
timu hizo katika awamu tatu ya michuano
hiyo na mechi za kufuzu katika kipindi hicho
hicho.
Miongoni mwa vitu ambavyo vilitiliwa mkazo
ni matokeo ya mechi za kufuzu kwa kombe la
dunia mwaka 2014.
Droo hiyo ambayo itabuni makundi manne
yanayoshirikisha timu moja moja kutoka kila
chungu itafanyika mjini malabo jumatano
usiku.
Ghana na Ivory Coast ni timu nyengine kubwa
huku washindi wa pili wa mwaka 3013
Burkina Faso wameorodheshwa katika kundi
la Pili.
2015 Nations Cup :Timu zilivyowekwa.
Pot 1: Equatorial Guinea, Ghana, Ivory Coast,
Zambia
Pot 2: Burkina Faso, Mali, Tunisia, Algeria
Pot 3: Cape Verde, South Africa, Cameroon,
Gabon
Pot 4: Guinea, Senegal, DR Congo, Congo
0 comments:
Post a Comment