728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, December 25, 2014

    KOCHA BAYERN:REUS NENDA MADRID USIJE BAYERN

    Kocha wa zamani wa klabu ya Bayern Munich Jupp Heynckes amemtaka winga wa klabu ya Borussia Dortmund Marco Reus kutojiunga na klabu ya Bayern na badala yake ajiunge na klabu ya Real Madrid ya Hispania.

    Jupp Heynckes amesema

    ``Kama kweli dau la Reus ni £20m na anataka kuhama basi ningemshauri aende Madrid kwakuwa pale atapata nafasi ya kucheza tofauti na Bayern ambapo nafasi yake ina wachezaji wanne mpaka watano hivyo huenda akawa na wakati mgumu sana hapo".
    Marco Reus ameonekana kuvivutia vilabu vingi vikubwa hasa baada ya hivi karibuni dau lake la uhamisho kuwekwa hadharani na kuwashangaza wengi.Baadhi ya vilabu vinavyomnyatia nyota huyo ni Liverpool,Chelsea,Real Madrid na Bayern Munich.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KOCHA BAYERN:REUS NENDA MADRID USIJE BAYERN Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top