Kiungo wa klabu ya West ham United Mcameroun Alexander Song amemuonya kiungo wa klabu ya Chelsea Cesc Fabregas kuwa asitegemee mtemremko katika mchezo wa ligi kuu utaopigwa mchana wa leo katika dimba la Stamford blidge.
Song 27 ambaye amecheza na Fabregas katika vilabu vya Arsenal na Barcelona amesema mchezo wa leo utakuwa ni wa kipekee sana kwake kutokana na uswahiba uliopo kati yake na Fabregas.
Anasema
`` Mimi na Fabregas ni kama ndugu.Nakumbuka wakati natua Arsenal wakati huo nikiwa na umri wa miaka 17 nilipaswa kwenda kulala hotelini lakini Fabregas akaniambia hapana njoo ulale kwangu.
Amenifundisha na kunishauri mengi lakini yote hayo yatasahaurika kwa muda pindi tutakapokutana mchana wa leo.Nataka kuhakikisha kuwa napambana naye na kisha kumshinda"Nimemwambia hata mke wangu.
Mechi hii na ile ya Arsenal jumapili ni mechi muhimu sana kwangu kwani zitanikutanisha na watu muhimu sana kwangu na furaha yangu itakuwa kubwa zaidi ikiwa nitafanikiwa kuisaidia West ham kushinda.
0 comments:
Post a Comment