Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amezitaja timu za Azam FC na
Yanga kuwa ndizo pekee zenye nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa msimu huu huku akizipa nafasi finyu timu za Simba na Mtibwa.
Akizungumza jana, Mayanja ambaye kikosi chake kiliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba Ijumaa iliyopita,alisema kuwa aina ya vikosi ambavyo
Yanga na Azam wanavyo ni silaha kubwa kwa timu mojawapo kati ya hizo kunyakua taji.
“Yanga na Azam FC wana vikosi vikubwa vyenye wachezaji wengi wenye ubora kulinganisha na timu nyingine zilizopo kwenye Ligi Kuu. Nadhani ukiniambia
nitaje timu gani nazipa nafasi ya kutwaa ubingwa, bila shaka nitakutajia Yanga na Azam.
“Ukiachilia mbali kuwa na vikosi vipana,timu hizo zina miundo mbinu mizuri ya kuziwezesha kufanya vizuri uwanjani...
Kwa mfano timu yetu ya Kagera
hatukucheza michezo ya kujipima nguvu kipindi ambacho ligi ilisimama. Hii ilisababishwa na timu kutokuwa na fungu la kutosha la kuleta timu ya kucheza nayo au kwenda mahali kucheza tofauti na hizo timu kubwa,” alisema Mayanja.
Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa timu yake, Mtibwa au Simba kutwaa ubingwa,alijibu kuwa timu hizo hazipi nafasi ya
kutwaa ubingwa labda itokee Azam na Yanga ziteleze kwenye mechi zao.
“Naomba niwe mkweli, sioni nafasi ya Kagera, Mtibwa au Simba kuwa bingwa msimu huu ila wanaweza kutwaa ikitokea
nafasi ya kufanya hivyo kama Yanga na Azam zitazembea,” alisema Mayanja.
0 comments:
Post a Comment