Kambi ya klabu ya Arsenal imepata faraja baada ya nyota wake wawili waliokuwa majeruhi Theo Walcott na Alex Oxlade Chamberlain kupona majeraha yaliyokuwa yakiwasumbua na sasa wako tayari kuivaa Liverpool jioni ya leo katika dimba la Anfield.
Walcott na Chamberlain wanaungana na mlinzi Calum Chambers ambaye anarejea baada ya kumaliza adhabu ya kukosa mchezo mmoja baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo ambao Arsenal iliambulia kipigo cha goli 3-2 toka kwa Stoke City.
Wakati huohuo Arsenal itaendelea kuwakosa wachezaji Aaron
Ramsey, Jack Wilshere, Mesut Ozil,
Laurent Koscielny, Tomas Rosicky, Abou
Diaby, Serge Gnabry na Mikel Arteta waliomajeruhi huku habari nyingine njema ikiwa ni kurejea kwa mlinda mlango David Ospina aliyekuwa nje kwa matatizo ya misuli.
0 comments:
Post a Comment