Nyota kinda wa klabu ya Arsenal Brooklyn Bechkam ameripotiwa kuwekewa mlinzi wa kumlinda maarufu kama bodyguard kokote anakokuwa ikiwa ni jitihada za kumlinda na watu wabaya.
Brooklyn 15 ambaye ni mtoto wa nyota wa zamani wa klabu ya Manchester United David Beckham hivi karibuni alijiunga na klabu ya Arsenal yenye maskani yake katika dimba la Emirates na kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha vijana cha U-16.
Kufuatia hatua hiyo Brooklyn amekuwa akilindwa na bodyguard maalumu ambaye hukaa katika benchi la Arsenal huku akiwa amevaa sare kama za wakufunzi (Makocha) wa klabu hiyo kila kikosi hicho kinapokuwa kikicheza mechi zake.
0 comments:
Post a Comment