Wafuatao ni makipa wanaolipwa vizuri ulimwenguni.
1-Iker Casillas
Kipa Iker Cassilas wa Real Madrid ndiye
anayeshika nafasi ya kwanza kwa
kulipwa mshahara mkubwa duniani
kwani kwa mwaka analipwa Pauni 6.3
milioni.
2-Manuel Neuer
Kipa wa Bayern Munich, Manuel Neuer
ndiye anayeshika nafasi ya pili kwa
makipa wanaolipwa zaidi kwa sababu
analipwa Pauni 5.6 milioni.
3-Petr Cech
Cech ni kati ya makipa bora katika Ligi
Kuu ya England. Petr Cech analipwa na
Chelsea mshahara wa Pauni 5.2 milioni
kwa mwaka.
4-Joe Hart
Kipa wa Manchester City, Joe Hart
ambaye amekuwa na misimu mizuri
analipwa mshahara wa Pauni 4.68
milioni kwa mwaka.
5-Pepe Reina
Kipa Pepe Reina wa Bayern Munich
anashika nafasi ya tano kwa makipa
wanaolipwa zaidi. Kiasi anacholipwa hivi
sasa na Bayern ni Pauni 4.16 milioni kwa
mwaka.
6-David De Gea
Kipa wa Manchester United, David De Gea
hivi sasa yupo katika kiwango cha juu
hivi sasa, klabu yake inamlipa mshahara
wa Pauni 3.64 milioni kwa mwaka.
7-Hugo lloris
Kipa wa Tottenham, Hugo Lloris hivi sasa
analipwa na klabu hiyo mshahara wa
Pauni 3.59 milioni kwa mwaka.
8- Gianluigi Buffon
Kipa mzoefu wa Juventus, Gianluigi ‘Gigi’
Buffon anashika nafasi ya nane katika
makipa wanaolipwa mishahara mikubwa.
Buffon analipwa mshahara wa Pauni 3.17
milioni kwa mwaka.
9-Claudio Bravo
Kipa huyu wa klabu ya Barcelona
analipwa na klabu hiyo Pauni 2.77
milioni kwa mwaka.
10-Salvatore Sirigu
Kipa anayefunga orodha ya makipa
wanaolipwa fedha nyingi ni kipa wa Paris
Saint Germain, Salvatore Sirigu. Kipa
huyu analipwa mshahara wa Pauni 2.6
milioni kwa mwaka.
0 comments:
Post a Comment