Manchester,England.
Kocha mkuu wa klabu ya Manchester United Mdachi Louis Van Gaal amewapiga marufuku nyota wa klabu hiyo kupaki magari yao karibu na mlango wa kutokea klabuni hapo kwa kisingizio cha kuwakwepa mashabiki.
Van Gaal amewataka wachezaji wa klabu hiyo kuachana na tabia hiyo na kujiweka karibu kabisa na mashabiki wao ambao wamekuwa wakiwaunga mkono katika hali zote.
Katika kuonyesha kuwa hana masihara kocha huyo amewaagiza nyota wake kupaki magari yao mbali zaidi na mlango wa kutokea klabuni hivyo waweze kupata muda mzuri zaidi wa kufahamiana na mashabiki wao pamoja na kusaini autographs.
Kali ilikuwa ni pale nyota Radamel Falcao ambaye alishushwa mbio mbio kutoka kwenye basi la klabu na kocha huyo ili akasaini Autographs za mashabiki waliokuwa wamejazana katika viwanja vya mazoezi vya Carrington mjini Manchester mapema wiki hii.
0 comments:
Post a Comment