Kuna kila dalili kuwa mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic (33) ameichoka klabu yake ya Paris Saint Germain na anataka kurudi Italia.
Ibrahimovic aliyejiunga na Psg mwaka 2012 akitokea Ac Milan inasemekana amechoshwa na maisha ya jiji la Paris na anataka kurudi Italia na safari hii ni katika klabu ya As Roma yenye maskani yake katika dimba la Olympico.
Habari kutoka vyombo vya habari vya Italia vinasema Ibrahimovic yuko tayari kushusha mshahara wake kwa kiwango kikubwa ili kukamilisha dili la kucheza Roma.
0 comments:
Post a Comment