Habari kutoa ndani ya klabu ya Arsenal zinadai kuwa mshambuliaji Lukas Podolski anajiandaa kuiacha klabu hiyo ya jiji la London na kujiunga na klabu ya Inter Milan ya Italia kwa mkopo wa miezi sita.
Habari za kuaminika zinadai kuwa tayari vilabu hivyo vimeshafikia makubaliano juu ya uhamisho wa mshambuliaji huyo aliyefanikiwa kufunga Arsenal magoli 31 katika michezo 81 kilichobaki ni kukamilisha masuala machache tu na hatimaye nyota huyo wa zamani wa Bayern Munich akakipigi katika dimba la Giussepe Meazza.
Klabu ya Inter itamtumia Podolski kwa kipindi cha miezi sita kisha ikiwa itakuwa imeridhishwa na kiwango chake italazimika kutoa ada ya kati ya £5-8m ili kummiliki moja kwa moja.
0 comments:
Post a Comment