728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, December 11, 2014

    SILVA MBIONI KUTUA ARSENAL

    Klabu ya Arsenal iko katika hatua nzuri za kumnasa kinda mahiri wa safu ya kiungo Mbrazil Lukas Silva  toka klabu ya Cruzeiro.Habari toka duru mbalimbali za kispoti zinasema kuwa klabu ya Arsenal imefanikiwa kuipiku klabu ya Real Madrid baada ya ofa yake ya 11.9m kukubaliwa na miamba hiyo ya Brazil Cruzeiro.

    Real Madrid ndiyo iliyokuwa ikipigiwa chapuo kumnasa kiungo huyo hodari lakini dau lake la paundi 9m limekataliwa na sasa nafasi hiyo adimum imeiangukia klabu ya Arsenal ambayo tayari inasemekana imeshaandaa jezi maalumu kwa ajili yake.Ikiwa Silva atafaulu kutua Arsenal atakuwa amefata nyayo za wabrazil wenzie kama Gilberto Silva,Neves Denilson,Edu na Julio Bptista.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SILVA MBIONI KUTUA ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top