Klabu ya Manchester United imemfungulia milango ya kutimka klabuni hapo kwa mkopo mwezi januari kinda wake Adnan Januzaj.
Januzaj (19) raia wa Ubelgiji ameshindwa kupata namba katika kikosi cha Manchester United kilicho chini ya kocha Mdachi Louis Van Gaal hasa baada ya ujio wa winga Angel di Maria kwa dau la rekodi akitokea klabu ya Real Madrid.
Januzaj ambaye mpaka sasa ameanza jumla ya michezo minne tu ya ligi huku akitokea benchi mara sita pekee anasemekana kuwindwa kwa mkopo na vilabu vya Hull City,Everton,Inter Milan na Real Sociedad inayonolewa na kocha wake wa zamani David Moyes.
0 comments:
Post a Comment