728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, December 30, 2014

    WAAMUZI BONGO HEBU CHAPENI ILALE

    Imeandaliwa na Paul Manjale
    0717 705548

    Wakati waingereza wakijidai kwa kuwa na Ken Aston muamuzi bora kabisa kuwahi kutokea duniani huku akiwaachia zawadi ya ugunduzi wa kadi za njano na nyekundu michezoni miaka ya 1960 baada ya lile sekeseke la mchezo wa kombe la dunia kati ya England na Argentina 1966 Wembley,Waitaliano wao hawalali wakaacha kumuota Pierluigi Collina je mimi na wewe tunalala na kumuota nani?Ni yupi kati ya waamuzi waliopo au waliopita bongo  anakufanya uitamani taaluma hii?Msomaji hili swali ni lako linakuhusu....

    Siandiki haya kwa ajili ya kumkera au kumkebehi muamuzi yoyote yule bali ni katika kuwekana sawa na kukumbushana tu kuhusu dhamana kubwa mliyonayo katika usitawi wa soka la taifa hili.Bila kuficha nakwazwa na pindisha pindisha ya mambo, nakwazwa na madudu yenu.

    Nijuavyo mimi uamuzi ni taaluma nyeti kama zilivyo taaluma nyingine nyingi,sasa kwanini mnaipaka taaluma hii matope?Hapa si ndipo mnapo patia kula,si ndipo panapo wapa majina mjini?Patendeeni haki basi.

    Hivi mpaka lini mtaendelea kutoka viwanjani mkiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi?Tena polisi wenye silaha kali na za moto?Kuna faida gani sasa ya kuwa muamuzi harafu ukategemea msaada wa polisi kurudi nyumbani aliko mke na wanao?Badilikeni pesa (Rushwa) isifanye muishi maisha ya sijui kesho itakuwaje.Maisha ya kukimbia kimbia kama wanariadha wa mbio ndefu.Tunaona Ulaya na kwingineko baada ya mechi waamuzi wanapewa mikono ya pongezi na wachezaji kwa kazi nzuri lakini nyinyi huku hadithi ni tofauti mnamaliza mpira mkiwa chini ya ulinzi wa polisi.Je,hayo ni maisha kweli?Hebu chapeni ilale muone kama kuna atakaye wasema au kuwanyooshea vidole kwa ubaya.

    Najua ugumu na changamoto zinazoikabili taaluma yenu lakini bado sioni sababu ya msingi inayofanya baadhi yenu mshindwe kutimiza majukumu yenu vizuri muwapo viwanjani.Sheria kumi na saba za soka ziko wazi kabisa sasa kwanini nyakati fulani fulani kwa makusudi mazima huwa mnaamua kuzipindisha?Hivi mtapungukiwa nini mkichezesha mpira kwa haki pasipo kumpendelea huyu na kumkandamiza yule?Badilikeni

    Ngoja niwaambie kitu labda mlikuwa hamjui.Mpira wa nchi hii unawahitaji mno nyinyi kwani bila nyinyi mambo hayaendi.Nyinyi ndiyo njia kweli na uzima mwenye kubisha na abishe tu.Vilabu hata visajili vipi kama maamuzi ya waamuzi yatabaki kuwa mabovu tutaishia kununa tu miaka nenda miaka rudi.Muda ndiyo huu amkeni tumechoka kuyaona madudu yenu viwanjani.Hebu tumieni taaluma yenu kwa uaminifu na umakini mkubwa kututoa hapa na kutupeleka kule ambako jicho la kila mtanzania linataka kupaona.

    Mwisho msichoke kujifunza,msichoke pia kubughuziwa na watu kama mimi ambao kiu na njaa yetu kubwa ni kuona mnafika mbali zaidi na zaidi.Hivi mnadhani Tanzania haipendi kuona mmoja kati ya waamuzi wake akichezesha fainali zijazo za kombe la dunia 2022 pale Qatar?Nitafuteni niwape jibu la swali hilo,nimemaliza kama vipi hepi nyu ia.2015 hiyooooo chapeni ilale...

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WAAMUZI BONGO HEBU CHAPENI ILALE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top