728x90 AdSpace

Wednesday, December 24, 2014

RODGERS AIKATAA PITCH YA ANFIELD

Pitch ya kuchezea ya Uwanja wa Anfield unaomilikiwa na klabu ya Liverpool utafanyiwa marekebisho msimu ujao kufuatia maombi ya kocha mkuu wa klabu hiyo Brendan Rogers.

Klabu hiyo imefikia maamuzi hayo kufuatia maombi ya mara kwa mara ya kocha huyo yalianza kutolewa mwaka 2012 pindi kocha huyo alipokabidhiwa mikoba ya kukinoa kikosi hicho.

Brendan anataka nyasi (pitch) za uwanja huo kuboreshwa akidai hali ilivyo sasa inazuia vijana wake kucheza mpira wa pasi maarufu kama one touch football.Katika kuonyesha msisitizo katika hilo Brendan amesema

``Nataka pitch ya Anfield iwe na ubora mzuri kama ile ya uwanja wa mazoezi wa Melwood.Pitch hii imezeeka haijafanyiwa marekebisho kwa kipindi kirefu sasa."

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: RODGERS AIKATAA PITCH YA ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Unknown