728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, December 11, 2014

    BALE,BENZEMA KUMPISHA AGUERO MADRID

    Klabu ya Real Madrid inasemekana kuwa katika mipango ya kuwapiga bei nyota wake wawili mahiri wa safu ya ushambuliaji Karim Benzema na Gareth Bale hapo mwakani.

    Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinadai kuwa uongozi wa klabu hiyo uko tayari kuwauza nyota hao ikiwa itatokea ofa yoyote nzuri kwa ajili ya nyota hao.Gareth Bale huenda akarejea England kujiunga na vilabu vya Chelsea ama Manchester United ambavyo kwa nyakati tofauti tofauti vimeonekana kummezea mate winga huyo mwenye kasi zaidi huku Benzema akitazamwa kwa karibu na vilabu vya Arsenal na Liverpool.

    Sababu za kuwepo mpango huo nim kwamba klabu ya Real Madrid inataka kukusanya kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kuwanasa nyota kama Sergio Aguero pamoja na winga wa Borussia Dortmund Marco Reus ili kuwa na safu kali zaidi ya ushambuliaji duniani ikimjumuisha Christian Ronaldo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BALE,BENZEMA KUMPISHA AGUERO MADRID Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top