728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, December 31, 2014

    CISSE:FA HAIJAKOSEA KUNIFUNGIA

    Mshambuliaji wa klabu ya Newcastle Papis Demba Cisse amesema chama cha soka cha England (FA) hakikukosea kumfungia kutocheza mechi tatu kwa kosa la kumpiga kiwiko mlinzi wa Everton Seamus Coleman.

    Akiongea na mtandao wa klabu hiyo Cisse ambaye aliisaidia Newcastle kuilaza Everton kwa mabao 3-2 ijumaa iliyopita amesema

    ``FA iko sahihi kunifungia hivyo kutokana na kosa hilo nachukua pia nafasi hii kumuomba radhi Coleman"

    ``Mimi siyo aina ya wachezaji wakorofi lakini katika mpira mambo haya hutokea"

    Kutokana na adhabu hiyo Cisse atalazimika kuukosa mchezo wa kesho dhidi ya Burnley,Leceister City na Chelsea hata hivyo mchezaji huo hatotumikia adhabu kutokana na kwenda Equatorial Guinea katika fainali za Afcon.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CISSE:FA HAIJAKOSEA KUNIFUNGIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top