Klabu ya Liverpool imeuaga mwaka 2014 kwa style ya aina yake baada ya kuifunga klabu ya Swansea City kwa magoli 4-1 katika mchezo mkali wa ligi kuu uliopigwa usiku wa jumatatu katika uwanja wa Anfield.
Liverpool ilipata magoli yake kupitia kwa mlinzi Alberto Moreno huku kiungo Adam Lallana akifunga mara mbili kabla ya kiungo Jonjo Shelvey akijifunga katika harakati za kuokoa.Goli la kufutia machozi la Swansea lilifungwa na kiungo Glyf Sirguardson.
Kufuatia ushindi huo Liverpool imechupa mpaka nafasi ya nane ikiwa na pointi 28 pointi 5 nje ya nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa.Liverpool itaivaa Leceister City mwaka mpya.
0 comments:
Post a Comment