Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya dirisha la usajili barani Ulaya lifunguliwe tayari mbio za kuwania wachezaji mbalimbali zimeshaanza huku tetezi nyingi zikiendelea kumiminika kwenye blog yako pendwa ya MchakaMchaka Viwanjani.
Kutoka ndani ya klabu ya Liverpool zinasema klabu hiyo inajipanga kumwachia kwa mkopo nyota wake Mario Balotelli kwenda klabu ya Napoli ya Italia baada ya kushindwa kuwika Anfield huku kukiwa na habari kuwa Liverpool inapanga kumsajili tena mshambuliaji Fernando Torres aliyeko kwa mkopo katika klabu ya Ac Milan ya Italia akitokea klabu ya Chelsea.
0 comments:
Post a Comment