Kocha mkuu wa klabu ya Borussia Dortmund Jurgen Klopp ameendelea kusisitiza kuwa hang'oki Dortmund licha ya klabu hiyo kuendelea kupokea vichapo kila uchao.
Klopp ambaye aliiongoza Dortmund jana kupokea kichapo cha 10 cha msimu cha bao 2-1 toka kwa klabu nyingine inayosuasua ya Werder Bremer amesisitiza bado ataendelea kupigania kibarua chake licha ya kufanikiwa kuvuna pointi 15 katika michezo 17 ya ligi ya Bundesliga.
Kichapo cha jana kimeiacha Dortmund katika nafasi ya pili mkiani huku ushindi wowote wa klabu ya Freiburg leo utaidondosha Dortmund mpaka mkiani kabisa mwa ligi hiyo ngumu duniani ambayo itasimama kwa wiki tatu kupisha sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya.
0 comments:
Post a Comment