Wakati klabu ya Liverpool ikihangaika kumshawishi nyota wake Raheem Sterling kumsaini mkataba mpya klabu ya Manchester City imeibuka na mpya baada ya kusema inapinga kubisha hodi klabuni hapo na ada ya £60m ili kumsajili nyota huyo wa pembeni.
Sterling amebakiza miaka miwili ili kumaliza mkataba na majogoo hao wa jiji la Liverpool huku kukiwa na sintofahamu hasa juu ya lini nyota huyo atakubali mkataba mpya na hatimaye kubaki klabuni hapo.
Mbali ya Manchester City vilabu vya Real Madrid na Bayern Munich navyo vimeonyesha nia ya kumnasa kinda huyo mahiri mzaliwa wa Jamaica.
0 comments:
Post a Comment