Baada ya kumpoteza kiungo wake Jack Wilshere kwa majeraha ya kifungo cha mguu na kuwa nje kwa miezi mitatu klabu ya Arsenal inapanga kutumia paundi 15m kumsajili kiungo mahiri wa klabu ya Newcastle Moussa Sissoko.
Sissoko 25 aliyejiunga na Newcastle mwezi januari 2013 akitokea klabu ya Toulouse ya Ufaransa amegeuka na kuwa tegemeo katika safu ya kiungo cha timu hiyo kiasi cha kuanza kufananishwa na kiungo wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa Patrick Vieira.
Arsenal inahitaji kiungo imara ili kuweza kuziba mapengo ya kumkosa Wilshere na mkongwe Mikel Arteta ambaye pia ni majeruhi.
0 comments:
Post a Comment