Mlinzi wa klabu ya Liverpool Muingereza Glen Johnson 30 mapema wiki hii amekataa mkataba mpya wa miaka miwili aliyopewa na klabu yake hiyo ya Merseyside.
Johnson ambaye yuko mwishoni mwa mkataba wake anapanga kutimkia klabu ya Roma ya Italia katika kipindi kijacho cha usajili barani Ulaya baada ya kukataa mkataba mpya uliokuwa na punguzo la asilimia 50 toka kwa klabu yake hiyo.
Ikiwa Johnson atafanikiwa kuhamia Roma atakuwa ni mchezaji wa pili wa kiingereza kuhamia Italia baada ya mkongwe Ashley Cole kufanya hivyo miezi michache iliyopita.
0 comments:
Post a Comment