SHABAN Ramadhan Kiemba ‘Shundu’
ambaye ni baba mdogo wa kiungo wa
Simba, Amri Kiemba, ameiomba klabu
hiyo kuachana na mwanaye kuliko kukaa
na kumpakazia maneno ya uongo
yanayomchafua katika jamii.
Kiemba pamoja na wachezaji wengine
wawili; Shaban Kisiga na Haroun
Chanongo, wamesimamishwa na uongozi
wa klabu hiyo kwa madai ya kucheza
chini ya kiwango na kuihujumu timu.
Shundu alisema: “Mwanangu (Amri
Kiemba) anateseka sana na hizo tuhuma,
si kweli kwamba anacheza chini ya
kiwango akiwa Simba, ni mfumo ndiyo
tatizo, madai wanayotoa viongozi si ya
kweli kabisa.
Akiwa Taifa Stars anacheza katikati, kazi
yake inakuwa kupeleka mashambulizi na
kusaidia kukaba kwa wakati fulani, akiwa
Simba wanamtumia pembeni, ni nafasi
mbili tofauti na huwezi kutegemea ufanisi
unaofanana.”
Kitaaluma Shundu ni kocha na amewahi
kuzifundisha timu kadhaa nchini kama
zikiwamo AFC na Palsons za Arusha,
Lipuli ya Iringa na Kahama United ya
Shinyanga.
“Ni bora wakamwacha tu, hajaniambia
kuwa anataka kwenda wapi lakini ni bora
akaenda Azam ama Yanga,” aliongeza.
0 comments:
Post a Comment