Dar es Salaam. Wakati beki wa kimataifa
kutoka Ivory Coast, Paschal Serge Wawa
akimwaga wino mkataba wa miaka
miwili kuichezea Azam, Simba imekataa
maombi ya Azam kumsajili kiungo Amri
Kiemba kwa mkopo.
Wakala wa mchezaji huyo aliwasili jana
akitokea Ivory Coat tayari kwa
mazungumzo ya mwisho na kusaini
mkataba na mmiliki wa timu hiyo,
Kampuni ya Said Salim Bakhressa.
Wawa ambaye tayari alishafanyiwa
vipimo vya awali vya uchunguzi wa afya
yake alikuwa akiichezea El Merreikh ya
Sudan, amechukua nafasi ya Ismailla
Diara kutoka Mali anayefungashiwa
virago na klabu hiyo kutokana na
kuonyesha uwezo mdogo.
Azam, tayari imeiandikia barua Simba
ikimtaka Kiemba ambaye amesimamishwa
na klabu hiyo kwa madai ya utovu wa
nidhamu.
Kwa upande wo, Azam wanamtaka
Kiemba kwa mkopo, kitu ambacho Simba
wamekigomea na kutaka wamnunue moja
kwa moja, wala si kumchukua kwa
mkopo.
Hadi sasa, Kiemba ana mkataba wa
mwaka mmoja wa kuitumikia klabu hiyo
ya Wekundu wa Msimbazi. Mmoja wa
viongozi wa Azam aliwarushia kijembe
Simba akisema:
“Simba ni watu wa ajabu, lengo lao ni
kumkomoa mchezaji kwani ni wazi
hawamtaki, lakini wanamng’ang’ania,
wakati hawatamtumii, sisi tupo tayari
kumchukua kwa mkopo.”
Awali, Kiemba alikuwa akiwaniwa na
Yanga msimu uliopita, lakini Simba
walipogundua hilo waliwahi na
kumsanisha mkataba wa miaka miwili.
0 comments:
Post a Comment