Mshambuliaji aliyeiwakilisha Ghana katika kombe lililopita la dunia nchini Brazil Majeed Waris 23 amepagawa baada ya taarifa kuibuka kuwa klabu ya Manchester United inamfuatilia kwa lengo la kumsajili.
Waris ambaye ni mshambuliaji tegemeo wa klabu ya Trabzonspor ya Uturuki amejikuta akipagawa baada ya kusikia kuwa kocha msaidizi wa Manchester United Ryan Giggs amekuwa akimfuatilia katika michezo mbalimbali akiwa na klabu hiyo ya Uturuki.
Amesema ``Manchester United ni klabu kubwa na kuhusishwa nayo ni jambo zuri sana"
``Nimesikia pamoja na kusoma habari mbalimbali kwakweli ni jambo zuri sana kusikia Manichester United wananifuatilia"
0 comments:
Post a Comment